9.5 C
New York

Papa Leo XIV amkwepa Trump

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

VITA ya maneno kati ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, na Rais wa Marekani, Donald Trump, imechukua sura mpya.

Safari hii, Papa Leo XIV amesema hana tatizo binafsi na Rais Trump na wala hataki kujibishana naye.

Papa Leo amekuwa mkosoaji wa sera za utawala wa Rais Trump, ikiwamo vita dhidi ya Iran aliyoiita kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Rais Trump naye amemjibu mara kadhaa Kiongozi huyo wa Dini, akimtaka kuachana na siasa kwa kuwa hakuna anachokijua.

Hivi karibuni akiwa kwenye ziara yake nchini Angola, Papa Leo alieleza kushangazwa na wanaotumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya vita, kauli iliyotafsiriwa kuwa ni ujumbe kwa Rais Trump.

Hata hivyo, Papa Leo amekanusha kuwa hakumlenga mwanasiasa huyo, akisema: “Bado imetokea kuonekana nilimlenga Rais, jambo ambalo sijihusishi lao kabisa.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img