MUNICH, Ujerumani
BAYERN Munich wameendeleza ubingwa wao Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) baada ya kutwaa taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo.
Bayern wamebaki na taji walilobeba msimu uliopita baada ya kuifunga Stuttgart mabao 4-2 katika mechi ya Aprili 19, 2026.
Mosi, Bayern wamemaliza mbio za ubingwa wakiwa wamebakiza mechi nne mkononi.
Pili, ni baada ya kuwa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya pointi 15, ambazo hakuna timu inayoweza kuzifikia katika mechi nne zilizobaki.
Tatu, wametwaa taji hilo wakiwa wamefungwa mechi moja pekee (dhidi ya Augsburg) tangu msimu huu uanze.
Nne, Bayern wametangazwa kuwa mabingwa wakiwa wamefunga jumla ya mabao 109 katika mechi 30 za Bundesliga.
Tano, jeuri yao ya upachikaji mabao inatokana na ‘kombinesheni’ kali ya washambuliaji watatu; Harry Kane, Luis Diaz na Michael Olise.
Sita, Kane ndiye kinara wa mbio za kuwania kitu cha ufungaji bora msimu huu wa Bundesliga, akiwa na mabao 32 katika mechi 27.
Saba, Bayern sasa watarejea dimbani Aprili 22, 2026 kuivaa Bayern Leverkusen katika nusu mtanange wa fainali ya Kombe la Ligi (DFB Pokal).
Nane, tayari timu hiyo imeshatinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo itavaana na PSG katika mchezo wa kwanza wa Aprili 28, 2026.
Tisa, Bayern ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa Bundesliga, ikifanya hivyo mara 35 (mara 13 ndani ya misimu 14 ya hivi karibuni).
Mwisho, ni taji la 10 la Bundesliga kwa nahodha wa kikosi, Joshua Kimmich, akiwa na vigogo hao wa soka la Ujerumani.


