7.6 C
New York

Rais kuongezewa muda yazua jambo Zimbabwe

Published:

HARARE, Zimbabwe

WANANCHI wa Zimbabwe wameonesha kutokuvutiwa na mpango wa Baraza la Mawaziri wa kuongeza muda wa rais kukaa madarakani.

Kwa mujibu wa Katiba ya sasa, rais atakuwa madarakani kwa miaka mitano, hivyo mabadaliko yataongeza hadi miaka saba.

Mpango huo, ambao bado haujawasilishwa Bungeni kama Muswada, unatajwa kulenga kumbakiza madarakani Rais Emmerson Mnangagwa hadi mwaka 2030.

Kwa upande wao, wanasiasa wa upinzani wameuita mpango huo kuwa ni ‘mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Katiba’ kwa lengo la kukilinda Chama tawala, Zanu-PF.

“Hayo mabadiliko yanayopendekezwa ni haramu na ni kinyume cha Katiba kwa kuwa yanakinzana na vifungu vyake,” amesema mwanasheria Tendai Biti.

Wakati huo huo, Augustine Kaswaurere, ambaye ni mwananchi, anasema: “Rais hapaswi kuongoza kwa muda mrefu ili aachie nafasi kwa wengine.”

Mnangagwa aliingia madarakani mwaka 2017 kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoung’oa utawala wa kidikteta wa miaka 30 wa Robert Mugabe.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img