9 C
New York

Merkel akanusha kutaka urais Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

OFISI ya aliyekuwa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, imekanusha taarifa zinazodai kuwa mwanamama huyo atagombea kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, macho ya wengi ni katika nafasi hiyo ya urais anayoshikilia Frank-Walter Steinmeier kwa sasa.

Tangu alipoachia nafasi ya Kansela, Merkel amekuwa hajihusishi na sasa kwa kile kinachotajwa kuwa ni hofu ya kuonekana ‘kivuli’ cha uongozi wa sasa.

Baada ya uvumi wa kutaka urais, Ofisi ya Merkel imeziita taarifa hizo kuwa ni uzushi unaopaswa kupuuzwa.

Kwa Wajerumani wengi, matamanio ni kuona nchi hiyo ikiandika historia ya kuwa na mwanamke katika kiti cha urais.

Hata hivyo, historia haioneshi kuwa kuna mwanasiasa aliyeshika nafasi hiyo akiwa ametokea kuwa Kansela, kama ilivyo kwa Merkel.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img