13.9 C
New York

Visual| Wakali 10 wa mauzo ya jezi Ulaya

Published:

LONDON, Uingereza

MAUZO ya jezi ni sehemu muhimu ya vyanzo vya mapato ya klabu za soka duniani kote, zikivuna mabilioni ya fedha kutokana na biashara hiyo.

Kwa mwaka 2025, wapo wachezaji waliofanya vizuri kwa jezi zao kuuzwa zaidi ndani na nje ya Bara la Ulaya. Ni akina nani hao?

Lamine Yamal

Idadi ya jezi zake zilizouzwa mwaka 2025 ni 1,315,000. Ni mwaka alioweka rekodi nyingi, ikiwamo ya mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lionel Messi

Jumla ya jezi 1,278,000 za supastaa huyo wa Inter Miami ya Marekani ziliuzwa mwaka 2025. Ni mwaka alioumaliza akiwa na mabao 35 na asisti 24 katika mechi za Ligi Kuu ya Marekani (MLS) pekee.

Robert Lewandowski

Kwa mwaka 2025, jezi 1,110,000 za staa huyo wa Barcelona ziliuzwa. Ni mwaka ambao klabu hiyo ilitwaa mataji yote matatu ya ndani. Lewandowski ana umri wa miaka 37 na zipo tetesi kuwa atatimkia Marekani.

Kylian Mbappe

Idadi ya jezi zake zilizouzwa mwaka 2025 ni 1,020,000. Ni kutokana na uwepo wa Mbappe klabuni hapo, Madrid iliongoza kwa mauzo ya jezi ( 3,133,000) duniani.

Vinicius Jr

Staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil. Jezi zake 992,000 ziliuzwa mwaka 2025, hivyo kuwa biashara nzuri kwa vigogo hao wa La Liga wanaoutumia Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Giorgian de Arrascaeta

Huyo ni staa wa Flamengo ya Brazil. Jezi zake 975,000 ziliuzwa mwaka jana baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu na Copa Libertadores akiwa amefunga mabao 18 na ‘asisti’ 14 katika mechi 33.

Cristiano Ronaldo

Jumla ya jezi 925,000 za nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno ziliuzwa mwaka jana. Ronaldo anayekipiga La Nassr ya Saudia, ana umri wa miaka 40 lakini bado hajaooteza ushawishi wake kwenye mauzo ya jezi.

Bruno Fernandes

Jezi 878,000 za kiungo huyo wa Manchester United ziliuzwa mwaka 2025. Kwa miaka mitano ya hivi karibuni, hakuna mchezaji aliyemzidi Bruno kwa kutengeneza nafasi za kufunga.

Harry Kane

Jezi zake 867,000 ziliuzwa mwaka jana. Kane, raia wa England anayekipiga Bayern Munich, alimaliza mwaka 2025 akiwa amefunga mabao 51.

Rodrygo

Kiungo wa pembeni (winga) wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil. Wakati fulani, alihusishwa na klabu za Liverpool na Manchester United. Kutokana na tetesi hizo, jezi zake 798,000 ziliuzwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img