7.6 C
New York

Mawani yanayosaidia wanaopoteza kumbukumbu

Published:

LOS ANGELES, Marekani

KAMPUNI maarufu ya Animorph Co-operative imemtambulisha mawani ya kisasa, ambayo yatawasaidia wanaokabiliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (dementia).

Hata hivyo, Szczepan Orlins, ambaye ni mhandisi wa Kampuni hiyo, amesema mawani hayo hayaji kumaliza moja kwa moja tatizo la kupoteza kumbukumbu, bali yatasaidia kwa kiwango cha kuridhisha.

Akielezea zaidi, mawani hayo yana kifaa maalumu cha akili-mnemba (AI) kinachofahamika kwa jina la Cross Sense, ambacho kitamsaidia mgonjwa wa aina hiyo kukumbuka majina ya watu aliowasahau awali.

Katika kumsaidia mtumiaji, mawani hayo yana uwezo wa kurekodi sauti na kuonesha picha ya matukio ya kila siku ili kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu.

Mwandishi wa habari wa Gazeti la mtandaoni la Times alijaribu kuvaa mawani hayo na kisha kuanza kupika chai, ambapo yaliweza kumkumbusha baadhi ya mambo, ikiwamo kuweka majani.

Kyamemsaidiawa mujibu wa wagonjwa watatu waliohojiwa na Gazeti la Times, wamedai kupata ahueni ya tatizo la kupoteza kumbukumbu tangu walipoanza kuvaa mawani hayo.

Miongoni mwao ni Rosalind Tranter, ambaye ni mstaafu wa taaluma ya udaktari wa meno, akisema mawani hayo kutokuwa ‘mzigo’ kwa kijana wake mwenye umri wa miaka 30.

Tranter anasema ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ulimfanya kusahau njia ya kurudi yumbani kila alipojaribu kwenda matembezi.

Kwa sasa, mstaafu huyo anatamani kuishi kwake, badala ya kumtegemea mtoto wake huyo aitwaye Joshua. “Ninachotaka ni kuishi kwenye nyumba yangu na si kuwa mzigo kwa mwanangu.

“Nafikiri teknolojia kama hii itanisaidia kutimiza ndoto hiyo. Inaweza kunisaidia kutokuwa tegemezi. Kwangu, imenipa faraja sana,” anasema.

Teknolojia hiyo itaanza kuingia sokoni mwishoni mwa mwaka huu, 2026, huku gharama ya mawani ikitarajiwa kuwa ni Pauni 700.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img