HARARE, Zimbabwe
WANANCHI wa Zimbabwe wamepokea kwa mwitiko mkubwa Bima ya Mazishi, ikiwa ni baada ya kushindwa kumudu gharama za Bima ya Afya.
Ifahamike kuwa Bima ya Mazishi inampa uhakika mwanachama wake kugharamiwa kila kitu baada ya kupoteza maisha.
Kwa walio wengi nchini Wazimbabwe, hasa wananchi wa kipato cha chini, hawamudu gharama za Bima ya Afya kwa kuwa ziko juu (Dola 200 kwa mwezi).
Hivyo, kwao wanaona ni bora Bima ya Mazishi, ambayo hugharimu chini ya Dola moja, ili kukwepa mzigo wa gharama wakati wa msiba.
Takwimu rasmi za Serikali zinaonesha kuwa asilimia 90 ya raia wa Zimbabwe, sawa na watu milioni 16, hawana uwezo wa kujigharamia Bima ya Afya.
Licha ya watumishi wa Serikali kuwa na uhakika wa Bima ya Afya, bado walio kwenye mfumo rasmi wa ajira nchini humo si zaidi ya watu 900,000.
Sekta ya Afya nchini Zimbabwe inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwamo bajeti isiyojisholeza, uhaba wa miundombinu, achilia mbali upungufu wa vitaa na wataalamu.


