7.6 C
New York

April Francis; Mrembo wa Wan-Bissaka anayekaribia kutupwa gerezani

Published:

LONDON, Uingereza

JINA la April Francis limetikisa vichwa vya habari za michezo nchini Uingereza baada ya mpenzi huyo wa beki wa West Ham United, Aaron Wan-Bissaka, kufunguliwa mashitaka yanayoweza kumtupa gerezani.

Bibiye huyo mwenye umri wa miaka 27, ashitakiwa kwa kumsabibishia ulemavu mpita njia aliyemgonga na gari Septemba, 2025.

kwa mujibu wa Gazeti la Sun la Uingereza.

Aprili anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati kesi yake itakaposikilizwa kwa mara ya kwanza Februari 2026.

Kusababisha majeraha kwa uzembe wakati wa kuendesha gari ni kosa kubwa nchini Uingereza, ambapo adhabu yake inaweza kuwa kifungo cha miaka mitano gerezani endapo utakutwa na hatia.

April na Wan-Bissaka wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2020 na kwa sasa wawili hao wana mtoto mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo kilichohojiwa na Gazeti la Sun, tukio hilo lilitokea mjini Brentwood.

“Ilikuwa ni saa 8:50 asubuhi, Jumanne ya Septemba 23, mwaka jana, ambapo polisi walipewa taarifa ya ajali iliyohusisha gari na mtembea kwa miguu katika Barabara ya Hartswood,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliongeza kuwa mtembea kwa miguu aliyegongwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 50 na ajali hiyo imemsababishia ulemavu.

Aidha, taarifa ya polisi ilieleza kuwa uchunguzi unaendelea juu ya ajali hiyo. “Tangu hapo, uchunguzi umekuwa ukiendelea,” ilieleza taarifa ya polisi.

Kwa wasiomjua, April alizaliwa Januari, 1995 jijini Manchester, ingawa ameendelea kuzifanya siri taarifa zinazowahusu wazazi na familia yake kwa ujumla.

Akiwa shule, alipenda zaidi kuwa mwanamitindo, ingawa aliangukia katika taaluma ya Kemia, ambayo tayari ana Shahada (Degree).

Licha ya taarifa za kipato chake kuwa siri, mpenzi wake, Wan-Bissaka, ni miongoni mwa wanasoka wenye mkwanja mrefu. Utajiri wake ni Dola za Marekani milioni 11.8.

Hata hivyo, April si mpenzi wa kwanza kwa Wan-Bissaka. Nyota huyo alikuwa na Rhianna Bentley, ambaye kuachana kwao kulisababisha wafikie hatua ya kupelekana mahakamani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img