5.7 C
New York

Tembo aliyekuwa balozi wa bia afariki

Published:

MOMBASA, Kenya

TEMBO maarufu nchini Kenya amefariki akiwa na umri wa miaka 54, akikumbukwa kwa heshima aliyokuwa nayo ya ubalozi wa kampuni ya bia ya Tusker.

Alifahamika kwa jina la Craig na taarifa rasmi zinaeleza kuwa mnyama huyo alifariki kutokana na umri mkubwa wa miaka 54 alipokuwa nao.

Craig alikuwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Amboseli iliyoko Kusini mwa Kenya, jirani na mpaka wa Tanzania.

Akisifika kwa mkonga wake mrefu na uzito wa kilogramu 45, Craig alipewa ubalozi wa bia ya Tusker mwaka 2021.

Utalii ni moja ya sekta nyeti katika uchumi wa Kenya, takwimu za maendeleo zikionesha kuwa huchangia asilimia 10 ya Pato la Taifa.

Kwa mwaka jana pekee, watalii zaidi ya milioni mbili waliripotiwa kuingia Kenya na kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img