5.7 C
New York

Tetemeko la ardhi laua watu wawili Mexico

Published:

MEXICO CITY, Mexico

WATU wawili wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Kusini mwa Mexico jana Januari 2, 2026.

Kwa mujibu wa kile kikichoelezwa na Shirika la Utangazaji la CBS, si tu vifo hivyo, bali pia watu wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.5, limetokea katika mji maarufu wa kitalii wa Acapulco, jirani na San Marcos.
Gavana wa Jimbo la Guerrero, Evelyn Salgado, amethibitisha kuwa mmoja ya waliopoteza maisha ni mwanamke mwenye umri wa miaka 50.

Kwa upande wake, Meya wa Mexico City, Clara Brugada, ameeleza kuwa mwingine aliyefariki ni mwanaume mwenye umri wa miaka 60.

Katika taarifa yake, Brugada amesema uzito wa tetemeko hilo la ardhi umesababisha watu wengine 12 kujeruhiwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img