CANBERRA, Australia
SERIKALI ya Australia imepanga kukazia zaidi sheria zinazopiga marufuku umiliki wa silaha za moto kwa wananchi wake.
Hatua hiyo inakuja baada ya shambulizi la kigaidi la hivi karibuni katika sherehe za Kiyahudi katika Ufukwe wa Bondi mjini Sydney. Watu 16 waliripotiwa kufariki.
Australia ni miongoni mwa mataifa yenye udhibiti mkubwa wa silaha kwa raia wake lakini sasa inataka kubana zaidi kupitia marekebisho ya sheria.
Kwa takwimu za sasa, ni watu 14 pekee kati ya 100 ndiyo wanamiliki silaha nchini humo lakini Waziri Mkuu wake, Anthony Albanese, amewasilisha mabadiliko ya sheria mbele ya Kikao cha Bunge ili kuona udhibiti unaongezwa zaidi.
Wakati hali ikiwa hivyo kwa Asutralia, utafiti wa mwaka wa 2918 unaitaja Marekani kuwa kinara wa nchi zenye idadi kubwa ya raia wanamiliki silaha. Kati ya watu 100 nchini Marekani, kuna silaha 120, ikifuatiwa na Yemen ambayo kati ya watu 100, kuna silaha 52.
Nchi zingine kwenye orodha hiyo ni New Caledonia (silaha 42 katika watu 100), Serbia (silaha 39 katika watu 100) na Montenegro (silaha 39 kati ya watu 100).


