5.7 C
New York

Wanajeshi sita wa UN wauawa Sudan

Published:

DARFUR, Sudan

UMOJA wa Mataifa (UN) umethibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake sita wanaolinda amani nchini Sudan wakati huu wa machafuko.

Kwa mujibu wa taarifa ya UN kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Antonio Guterres, wapiganaji sita hao ni raia wa Bangladesh.

Taarifa ya Guterres imeeleza kuwa mbali ya sita kuuawa, wengine nane wamejeruhiwa baada ya kambi yao mjini Kadugli kushambuliwa na ndege isiyo na rubani.

Kwa upande mwingine, huku Guterres akihusisha shambulizi hilo n uhalifu wa kivita, Serikali ya Sudan imewataja wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) kuhusika.

Hata hivyo, RSF kupitia taarifa yao waliyochapisha katika mtandao wa Telegram wamekanusha madai hayo ya Serikali.

Wakati huo huo, Rais wa mpito wa Bangladesh, Muhammad Yunus, ameeleza kusikitishwa na taarifa za wanajeshi wake kuuawa katika operesheni ya kulinda amani nchini Sudan.

“Serikali ya Bangladesh iko pamoja na familia zao katika kipindi hiki kigumu,” alisema Rais huyo.
Sudan imekuwa kwenye mtanziko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili mfululizo tangu Aprili, 2023, kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa RSF.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img