5.7 C
New York

Wabunge Kenya wawajia juu wanajeshi Uingereza

Published:

NAIROBI, Kenya

BUNGE la Kenya limewashutumu wanajeshi wa Uingereza likiwataja kufanya vitendo vya udhalilishaji walipokuwa kwenye mafunzo nchini humo. Kwa miaka mingi, vikosi vya jeshi vya Uingereza vimekuwa vikiendesha mafunzo nchini Kenya kupitia programu ya pamoja ya British Army Training Unit in Kenya (Batuk).

Kupitia programu hiyo, wanajeshi zaidi ya 1,000 wa Kenya hupokea mafunzo ya wenzao wa Uingereza kila mwaka. Sasa, kwa mujibu wa ripoti ya Bunge, wanajeshi hao walijihisisha na vitendo vya unyanyasaji wa kingono, mauaji, uharibifu wa mazingira, na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ripoti hiyo imesema wanajeshi wa Uingereza walifanya hayo katika jamii za Laikipia na Samburu zinazopakana na kambi ya mafunzo.

Kwa upande mwingine, wanajeshi wa Uingereza wameshutumiwa kwa kugoma kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi huo uliofanywa na Bunge. Wakati huo huo, Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya nao umeahidi kufanya uchunguzi juu ya madai hayo ya ripoti hiyo ya kurasa 94.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img