5.7 C
New York

Tume yaundwa kuchunguza ajali ya moto

Published:

VICTORIA, Hong Kong

KIONGOZI wa Hong Kong, John Lee, ameunda Tume ya kuchunguza chanzo cha ajali ya moto iliyosababisha vifo vya watu takribani 151. Jumatano ya wiki iliyopita, sehemu kubwa ya Jengo la Mahakama la Wang Fuk, ambalo wakati huu limekuwa kwenye ukarabati mkubwa, iliteketea kwa moto.

Wakati huu jitihada za uokoaji zikiendelea, inasadikika kuwa huenda idadi hiyo ya vifo ikaongezeka zaidi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa. Hata hivyo, taarifa ya awali ya wakosoaji ilidai kuwa licha ya gharama kubwa ya ukabati, vifaa vya kuzuia majanga ya moto vilikuwa vimewekwa kwenye jengo hilo havikuwa na viwango.

Kutokana na ajali hiyo, watu takribani 13, wakiwamo wakurugenzi wa kampuni ya ujenzi iliyosimamia ukarabati, wanashikiliwa na vyombo vya dola.

Moto huo unatajwa kuwa ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea Hong Kong kwa kipindi cha miaka zaidi ya 70 lakini Lee alikwepa kujibu alipoulizwa kama anapaswa kujiuzulu kutokana na ajali hiyo.

Na badala yake, kiongozi huyo alisema Kamati iliyoundwa italeta mageuzi makubwa na itakuja na suluhisho la majanga ya aina hiyo katika siku za usoni. “Ndiyo, ni janga na ni moto mkubwa. Tunahitaji mabadiliko. Ndiyo, tumegundua udhaifu katika baadhi ya maeneo. Ndicho tunachopaswa kufanyia kazi, kuhakikisha haturudii makosa,” alisema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img