5.7 C
New York

Watu 20 watekwa Nigeria, wamo mchungaji na bibi harusi

Published:

ABUJA, Nigeria

Watu wenye silaha wamewateka nyara takriban watu 20, wakiwemo mchungaji wa kanisa na bibi harusi, katika mashambulizi mawili tofauti yaliyotokea nchini Nigeria katika kile kinachoonekana kuwa ongezeko jipya la matukio ya utekaji nyara.

Tukio la kwanza lilitokea Jumapili katika Kanisa jipya la Cherubim na Seraphim, jimboni Kogi katikati mwa nchi, ambako washambuliaji walivamia ibada, wakapiga risasi hovyo na kusababisha waumini kukimbia kwa hofu. Katika tafrani hiyo, watekaji walimchukua mchungaji wa kanisa hilo, mkewe pamoja na waumini wengine kadhaa.

Katika shambulio la pili, lililotokea usiku wa kuamkia jana katika jimbo la Sokoto kaskazini mwa Nigeria, bibi harusi na wasimamizi wake walitekwa nyara. Kwa mujibu wa taarifa za AFP, mtoto mmoja, mamake pamoja na mwanamke mwingine pia waliangukia mikononi mwa watekaji.

Mashambulizi dhidi ya shule, maeneo ya ibada na jamii yameongezeka katika kanda za kaskazini na kati nchini humo, hali inayoongeza wasiwasi kuhusu usalama na uwezo wa mamlaka kukabiliana na wimbi la utekaji nyara nchini Nigeria.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img