5.7 C
New York

Mama jela maisha kwa kuua, kuficha miili ya watoto

Published:

WELLINGTON, New Zealand
MWANAMKE mmoja nchini New Zealand amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka ya kuua watoto wake wawili, kisha kuficha miili yao katika mifuko.
Hakyung Lee aliua watoto hao mwaka 2018, mmoja akiwa na umri wa miaka nane na mwingine miaka sita.
Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa mahakamani, aliwaua kwa kuwapa juisi aliyokuwa ameweka sumu aina ya ‘nortriptyline’.

Miili ya watoto hao ilikuja kuonekana mwaka 2022 mjini Auckland. Kutokana na mauaji hayo, atalazimika kutumikia miaka walau 17 ndipo anaweza kufikiriwa katika nafasi za msahama.
Lee mwenye umri wa miaka 45, amedai kuwa alitenda kosa hilo akiwa amevurugwa kiakili baada ya kifo cha mumewe.
Hata hivyo, kwa mujibu wa waendesha mashitaka, mwanamke huyo anawajibika kwa kosa kwani alikwepa majukumu ya kulea watoto akiwa peke yake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img