12.7 C
New York

Israel yamuua kiongozi wa Hezbollah

Published:

JARUSALEM, Israel
IMERIPOTIWA kuwa kiongozi mwandamizi wa Kundi la Hezbollah la Lebanon, Haitham Ali al-Tabtabai, ameuawa katika shambulizi lililofanywa na vikosi vya Israel.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Lebanon, shambulizi hilo limesababisha vifo vya watu watano na wengine 28 kujeruhiwa.
Taarifa yake imeeleza zaidi, kwamba Israel ilishambulia jengo lililopo katika Wilaya ya Dahieh.
Kwa upande wake, uongozi wa Hezbollah umethibitisha kifo cha kiongozi wake, Tabtabai,
Aidha, Hezbollah wameionya Israel ikiiambia kwa sasa imevuka mpaka katika mashambulizi yake.
Hezbollah, Kundi la kigaidi kama linavyotajwa na Marekani na washirika wake, limekuwa likihusishwa kupata msaada kutoka Iran.
Hata hivyo, Serikali ya Israeli imedai kuwa shambulizi lake limelenga kusambaratisha jitihada za Hezbollah kujenga ngome zake za kigaidi.
Akizungumza baada ya shambulizi hilo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema:
“Katika utawala wangu, Serikali ya Israel haitaruhusu Hezbollah iwe na nguvu, haitaruhusu Kundi hilo kuwa tishio kwa Serikali ya Israel.”
Pia, Netanyahu aliipa angalizo Serikali ya Lebanon akiitaka kuwekeza nguvu katika kukabiliana na Hezbollah.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img