5.7 C
New York

Waasi wavamia shule, wateka watu 300

Published:

LAGOS, Nigeria
WATU wenye silaha waliodhaniwa kuwa ni miongoni mwa vikundi vya waasi wameteka watu 300, wakiwamo wanafunzi, baada ya kuvamia shule ya Kikatoliki.
Idadi hiyo ya waliotekwa ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya uhalifu wa vikundi vya waasi nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha Wakiristo cha Nigeria, waliotekwa ni wanafunzi 303 na waalimu 12 katika Shule ya St Mary mjini Papiri.
Awali, idadi ya wanafunzi waliokuwa wameripotiwa kutekwa ilikuwa 215 lakini sasa imeongezeka.
Mmoja ya mashuhuda ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa wapwa zake wawili, mmoja wa miaka sita na mwingine 13, nao walitekwa.
Hata hivyo, mamlaka zimeitupia lawama shule hiyo zikisema ilipuuza amri ya kutoruhusu wanafunzi kuendelea kulala, na badala yake warudi nyumbani baada ya masomo.
Mamlaka zimeeleza kuwa amri hiyo inatokana na hali mbaya ya usalama katika maeneo mengi nchini Nigeria.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img