10.1 C
New York

Mafuriko yaua watu 90

Published:

HANOI, Vietnam
WATU takribani 90 wamepoteza maisha na wengine 12 hawajulikana walipo kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko nchini Vietnam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, mvua kubwa hiyo imesababisha uharibifu wa makazi 186,000 nchini humo.
Katika hatua nyingine, taarifa hiyo inaeleza kuwa mifugo zaidi ya milioni tatu imepoteza maisha.
Mbali ya maafa hayo, watu wapatao 258,000 wamekosa huduma ya umeme, huku ukiwapo uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Hata hivyo, madhara yamejitokeza zaidi katika Jimbo la Dak Lak, ambako vifo vya watu zaidi ya 60 vimeripotiwa.
Mafuriko yanakuja wakati ikiwa ni miezi miwili tu tangu Vietnam ilipokumbwa na janga la kimbunga.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img