KYIV, Ukraine
WATU takribani 26, wakiwamo watoto watatu, wamepoteza maisha katika shambulizi la Urusi nchini Ukraine.
Vifo hivyo vimetokana na shambulizi la ndege isiyo na rubani katika majengo mawili Magharibi mwa Mji wa Ternopil.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya usalama nchini Ukraine, shambulizi hilo limejeruhi watu 93, wakiwamo watoto 18.
Shambulizi hilo limetajwa kuwa ni miongoni mwa yale makubwa zaidi kutekelezwa na Urusi tangu ilipoivamia Ukraine mwaka 2022.
Katika video aliyosambaza Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, jengo lenye ghorofa tisa linaonekana likiwa limesambaratishwa.
Ukraine imekuwa ikilaani mashambulizi ya Urusi yanayolenga maeneo nyeti, ikiwamo miundombinu ya usafiri.
Published:


