9.3 C
New York

Nicki Minaj amuunga mkono Rais Trump

Published:

LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI wa Hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, ameiunga mkono kauli ya Rais Donald Trump aliyedai kuwa waumini wa Dini ya Ukiristo nchini Nigeria wamekuwa wakiuawa.
Rais Trump amekuwa akiishutumu Serikali ya Nigeria kwa kushindwa kushughulikia hilo na wakati mwingine akitishia kuivamia kijeshi ili kukomesha matukio hayo.
Hata hivyo, tofauti na mtazamo wake, wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema si kweli kwamba ni Wakiristo pekee wanaolengwa na vikundi vya magaidi nchini Nigeria.
Mathalan, katika tukio la wiki hii, watu wawili walipoteza maisha baada ya kanisa kushambuliwa mjini Kwara, pia wasichana 25 waliotajwa kuwa ni Waislam walitekwa.
Kwa upande wake, akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na Marekani, Minaj alisema: “Nchini Nigeria, Wakiristo ni wahanga wakubwa.
“Makanisa yamekuwa yakichomwa, familia zimekuwa zikitengenganishwa… Ni kwa vile tu wao ni Wakiristo.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img