5.5 C
New York

Baraza jipya la Mawaziri ‘surprise’, walioachwa, wapya na waliobaki

Published:

Na Mwandishi Wetu,Gazetini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza baraza jipya la mawaziri, akiunda jumla ya wizara 27, mbili zikiwa mpya ambazo ni Ofisi ya Rais na Maendeleo ya Vijana.

Rais Samia ametangaza baraza hilo leo, Novemba 17, 2025 mbele ya waandishi wa habari, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

Katika orodha ya mawaziri na manaibu waziri watakaoongoza wizara hizo, majina mapya yamejitokeza, pia wengine wakiendelea kubaki katika wizara zao, kuna waliohamishwa na waliondolewa kabisa.

Jumla ya mawaziri nane wamewekwa kando katika baraza hilo jipya. Walioachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, pamoja na mawaziri: Hussein Bashe (Kilimo), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Jenista Mhagama (Afya), Dk. Seleman Jafo (Viwanda na Biashara), Dk. Pindi Chana (Maliasili na Utalii), Dk. Damas Ndumbaro (Katiba na Sheria) na Stergomena Tax (Ulinzi).

Katika Baraza hilo jipya aliyechukua nafasi ya Dk. Biteko Wizara ya Nishati ni Deogratius Ndejemb, Naibu Waziri ni Salome Makamba, Mrithi wa Bashe Wizara ya Kilimo ni Daniel Chongolo na Naibu Waziri David Silinde. Wizara ya Mambo ya Ndani iliyokuwa chini ya Bashungwa amerejeshwa George Simbachawene, huku Naibu Waziri akiwa ni Denis Londo.

Rais Samia amemteua Rhimo Nyansao kuwa Waziri wa   Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambayo ilikuwa ikiongozwa na Stergomena Tax, Maliasili na Utalii iliyokuwepo Pindi Chana kwa sasa Waziri wake ni Ashatu Kijaji, Naibu ni Hamad Hassan Chande. Viwanda na Biashara iliyokuwa ya Jafo Waziri wake ni Judith Kapinga na Naibu Patrobas Katambi, nafasi ya Ndumaro Katiba na Sheria imechukuliwa na Juma Homera na Naibu Zainab Athuman Katimba.

Mawaziri wapya ni Balozi Hamis Mussa Omary ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha akichukua nafasi ya Dk. Mwigulu Nchemba ambaye wiki iliyopita aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Paul Makonda Naibu Waziri wa Habari na Michezo akiwa na Hamis Mwinjuma ‘FA’ huku Waziri akiwa Palamagamba Kabudi.

Joel Nanauka kuwa Waziri wa Vijana, Wizara ipo chini ya Ofisi ya Rais, Wanu Hafidhi ambaye ni Bunge wa Makunduchi Zanzibar kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akimsaidia Profesa Adolf Mkenda, Juma Homera kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,

Sura nyingine mpya ni Balozi Dk. Bashiru Ally (Waziri wa Mifugo na Uvuvi) na Naibu Waziri wake ni Ng’wasi Kamani, Daniel Chongolo (Waziri wa Kilimo), Rahma Riyadh Kisuo kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ajira, kazi na Mahusiano.

Wizara ya Ujenzi itaendelea kuwa chini ya Abdallah Ulega na naibu wake ni Geoffrey Kasekenya, Profesa Makame Mbarawa anaendelea kuwa Waziri wa Uchukuzi na Juma Awezo anaendelea Wizara ya Maji na naibu wake Mhandisi Kundo Mathew.

Dk. Dorothy Gwajima amebaki Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, naibu wake ni Maryprisca Mahundi, Wizara ya Madini anaendelea kuwa Anthon Mavunde, naibu wake Dk. Steven Kiruswa na Profesa Kitila Mkumbo Waziri, Ofisi ya Mipango na Uwekezaji.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo anaendelea kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, manaibu wake ni Dk. Ngwaru Maghembe na James Ole Millya. William  Lukuvi ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu

Wizara ya afya ni Mohamed Mchengerwa, Angela Kairuki kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Waziri Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni Ridhiwani Kikwete.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img