21.6 C
New York

Sikia hii ya unga wa protini kujenga mwili, kupunguza uzito

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MARA kadhaa baadhi ya wataalamu wa mazoezi ya viungo huko mitandaoni, hasa TitTok na Instagram wamekuwa wakihimiza matumizi ya protini kwa wingi.

Ushauri huo umeongeza idadi ya bidhaa za protini, ukiwamo unga, ambao vijana wengi wanaofanya mazoezi ya ‘gym’ wamekuwa wakiutumia ili kupunguza uzito au kujenga misuli (six packs).

Si tu unga, vijana wengi wa Uingereza hutumia pia vyakula na vinywaji vyenye protini nyingi, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2024.

Sasa, ni kweli wataalamu wa afya wanakubaliana kuwa protini mwilini ina mchango mkubwa, ikiwamo kujenga na kuimarisha misuli.

Hata hivyo, tafiti zaidi ya 350 zinaonesha kuwa matumizi kidogo ya protini yanasaidia kupunguza uzito, kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na magonjwa ya moyo, pamoja na kuongeza muda wa kuishi.

Moja ya tafiti hizo ni huu wa Chuo Kikuu cha Wisconsin–Madison, ukieleza kuwa matumizi ya kiwango kidogo cha protini yana mchango mkubwa katika mfumo wa ukuaji, pia kudhibiti seli zinazosababisha kuzeeka haraka.

Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la afya la Cell Press Blue umeainisha kuwa miwili wa kiumbe hai una homoni aina ya fibroblast growth factor 21.

Homoni hizo huongeza matumizi ya nishati mwilini na kuimarisha udhibiti wa kiwango cha sukari. Pindi protini inapokuwa ndogo, homoni hizo huongezeka na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema utafiti huo ulijikita kwa wadudu, wakiwamo panya, hivyo matokeo yake hayawezi kuwa na uhalisia wa moja kwa moja kwa mwili wa binadamu.

Hivyo, wataalamu wanashauri kwamba licha ya umuhimu wa protini mwilini, matumizi yake yanapaswa kuwa ya kiwango cha wastani, wengine wakionya kuwa kuzidisha kunaweza pia kuathiri ufanisi wa viungo muhimu vya mwili, ikiwamo figo.

“Ni wazi kuwa protini ina faida ya kujenga misuli lakini watu wengi wanatumia kiasi kikubwa, ikilinganishwa na miili inavyohitaji, jambo ambalo lina madhara kwa afya.

Mtaalamu huyo anasema kiwango kikubwa cha protini kinahitajika kwa wajawazito na wazee,” anasema Dudley Lamming, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison.

Related articles

Recent articles