27.8 C
New York

Maandamano kupinga mauaji ya Meya yaendelea Mexico

Published:

MEXICO City, Mexico
BADO maelfu ya raia wa Mexico wameendelea kuingia barabarani wakishinikiza mabadiliko makubwa kwenye vyombo vya usalama.
Ikumbukwe, hasira za waandamanaji, ambao wengi wao ni vijana, zilitokana na kuuawa kwa aliyekuwa Meya wa Uruapan, Carlos Manzo.
Carlos alifariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana, tukio lililotokea Novemba Mosi, mwaka huu, lakini waandamaji wanaamini aliuawa na Serikali.
Kwa mujibu wa waandaamanaji, vyombo vya dola vimeshindwa kumaliza kero ya hali mbaya ya usalama nchini humo na kusababisha kifo cha mwanasiasa huyo.
Katika hatua nyingine, baadhi ya waandamanaji wameonekana wakifika hadi kwenye uzio wa nyumba anayoishi Rais Claudia Sheinbaum.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, polisi 100 na raia 20 wamejeruhiwa katika maandamano hayo.

Related articles

Recent articles