INSTANBUL, Uturuki
NDEGE ya kijeshi ya mizigo nchini Uturuki imepata ajali ikiwa na abiria 20, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.
Taarifa imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea mpakani mwa Azerbaijan na Georgia, ingawa hakuna Wizara haijaeleza madhara yaliyojitokeza.
Wizara ya Ulinzi imeeleza kuwa ndege hiyo aina ya C-130 ilikuwa ikirejea Uturuki ikitokea Azerbaijan.
Kwa mujibu wa mamlaka ya anga ya Georgia, ndege hiyo ilipotea kwenye rada baada ya kupoteza mawasiliano, kisha kuanguka umbali wa kilometa 5 kutoka Azerbaijan.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameunga na mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, kueleza kusikitishwa na taarifa za ajali hiyo.
Naye balosi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack, ametumia ukurasa wake wa X kuandika: “Tunapeleka salamu zetu za rambirambi kwa familia za wafia, jeshi na watu wa Uturuki.”
Ngege za mizigo aina ya C-130 hutengenezwa Marekani na zinatumiwa na jeshi katika nchi nyingi duniani.
Published:


