12.5 C
New York

Waasi Sudan watangaza kuteka mji

Published:

DARFUR, Sudan
WAPIGANAJI wa kikundi cha waasi cha Rapid Support Forces (RSF) wametangaza kuuteka Mji wa el-Fasher ulioko Magharibi mwa Sudan.
Kwa miezi takribani 18, wapiganaji wa RSF walikuwa wameuzunguka Mji wa el-Fasher.
Aidha, hatua ya kuuteka si tu ni pigo kubwa kwa wanajeshi wa Serikali, bali pia itachochea vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini humo.
Taarifa hizi mpya zinakuja huku zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu waasi wao walipotangaza kuyateka makazi ya jeshi ya 6th Division na kuharibu magari, Pamoja na kuchukua silaha.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limethibitisha kuwapo kwa video zinazowaonesha wapiganaji wa RSF wakiwa ndani ya kambi hiyo ya jeshi.
Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa (UN) umelinyooshea kidole Kundi la RSF ukilitaja kuhusika katika uhalifu dhidi ya binadamu nchini Sudan.
Sudan imekuwa kwenye mateso ya vita tangu mwaka 2023, chanzo kikiwa ni makamanda waandamizi wa RSF na wale wa jeshi la Serikali kugombea madaraka ya kuiongoza nchi hiyo.
Kutokana na machafuko yanayoendelea, watu zaidi ya 150,000 wameripotiwa kupoteza maisha, huku wengine milioni 12 wakilazimika kuyakimbia makazi yao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img