12.5 C
New York

Rais ‘mzee’ zaidi duniani ashinda tena Uchaguzi Cameroon

Published:

YAOUNDE, Cameroon
AKIWA na umri wa miaka 92, Paul Biya ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Cameroon uliofanyika hivi karibuni.
Biya amerejea madarakani na huu unakuwa muhula wake wa nane kuliongoza Taifa hilo la Afrika ya Kati lenye watu zaidi ya milioni 29.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi, ameshinda kwa asilimia 53.7 ya kura, akimpiku mgombea wa upinzani, Issa Tchiroma Bakary, aliyepata asilimia 35.2.
Hata hivyo, Uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 12 umeripotiwa kugubikwa na ghasia za hapa na pale.
Mamia ya wafuasi wa Tchiroma Bakary wameonekana wamepinga matokeo hayo kwa kuandamana katika miji mbalimbali na wakati mwingine wakipigana na polisi.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, watu takribani wanne waliripotiwa kupoteza maisha katika maandamano ya mjini Douala. Pia, jana zilikuwapo taarifa kuwa watu wawili wamefariki kwa kupigwa risasi na polisi.
Ikumbukwe, hata kabla ya matokeo kuanikwa jana, tayari Tchiroma Bakary alishajitangaza kuwa ndiye Rais mpya wa Cameroon na kumtaka Biya akubali matokeo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img