YAMOUSSOUKRO, Ivory Coast
HATIMAYE Alassane Ouattara amechaguliwa tena kuwa Rais wa Ivory Coast, ukiwa ni muhula wake wa nne madarakani.
Ouattara mwenye umri wa miaka 83, amepata ushindi wa kishindo wa asilimia 89.8 ya kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.
Aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za urais ni mfanyabiashara Jeal-Louis Billon, ambaye hata hivyo aliambulia asilimia 3.09 tu ya kura zilizopigwa.
Hata hivyo, wakosoaji wameubeza ushindi huo wakiamini kuwa kwa kiasi kikubwa umetokana wa Rais Ouattara kukosa wapinzani wenye nguvu.
Ni baada ya baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi, ambao walionekana wangempa upinzani mkali, kuzuiwa kugombea kiti cha urais.
Miongoni mwao waliowekewa kizingiti na kushindwa kugombea ni rais wa zamani, Laurent Gbagbo.
Mke wa zamani wa Gbagbo, Simone, ambaye aliruhusiwa kugombea, aliambulia asilimia 2.42 tu ya kura.
Published:


