12.5 C
New York

Usiyoyajua kuhusu ICC; Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MWAKA jana, Ras Donald Trump alitangaza kuiwekea vikwazo Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kwa kile alichodai kuwa Mahakama hiyo imekuwa haitendi haki dhidi ya Marekani na washirika wake, Israel.
Vikwazo vya Marekani kwa ICC vilihusisha kuwanyima msaada wa fedha na kuwazuia kuingia nchini humo maofisa wa Mahakama hiyo.

ICC ni nini? Ni Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ambayo inahusika na mashitaka ya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. Makao Makuu ya Mahakama hiyo yako mjini The Heague, Uholanzi. Ilianzishwa mwaka 2002, lengo likiwa ni kuwawajibisha kwa kuwafungulia mashitaka viongozi wanaotumia vibaya madaraka.

Kwanini Marekani imeiwekea vikwazo ICC? Novemba, mwaka jana, itakumbukwa kuwa ICC iliamuru kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kuhusika katika uhalifu dhidi ya binadamu katika Ukaenda wa Gaza.

Agizo hilo la kukamatwa liliwahusu pia Waziri wa ulinzi wa zamani wa Israel, Yoav Gallant, pamoja na kiongozi wa Kundi la Hamas, Mohammed Deif. Katika ziara ya Netanyahu mjini Washington DC, Serikali ya Marekani ikatangaza kuiwekea vikwazo ICC na kusema Mahakama hiyo imekuwa na maamuzi yanayoinufaisha Hamas.
Rais Trump alisema ICC imekuwa ikipuuza jitihada za Israel kujitetea dhidi ya mashambulizi ya Hamas, pia ‘ikipotezea’ makosa yanayofanywa na Iran.

Hata hivyo, Trump siyo kiongozi wa kwanza wa Marekani kuikosoa ICC. Rais wa zamni wa Marekani, Joe Biden, naye alipinga hatua ya Mahakama hiyo kutaka Netanyahu akamatwe. Marekani, licha ya ushawishi wake mkubwa katika siasa za ulimwengu, si mwanachama wa ICC. Ni kama ilivyo kwa mshirika wake wa karibu, Israel.

Hata hivyo, Marekani imekuwa ikishiriki katika mashitaka kadhaa ya ICC. Ni kama Rais Joe Biden alivyoamuru vyombo vyake vya usalama kutoa ushahidi wa namna Urusi ilivyohusika katika uhalifu wa kivita nchini Ukraine.
Aidha, ukiacha Marekani na Israel, mataifa mengine ambayo si mwanachama wa ICC ni pamoja na China, India, Pakistan, Indonesia na Uturuki.

Mwaka 2012, ICC ilimfungulia mashitaka kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga. Alishitakiwa kwa kuajiri watoto kwenye Kundi lake na alihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani.

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, naye aliwahi kufikishwa kwenye Mahakama hiyo mwaka 2011, akikabiliwa na mashitaka ya mauaji na ubakaji wakati wa machafuko nchini humo. Aliachiwa baada ya kukutwa hana hatia.

Lakini, wakati ICC ikikosolewa kwa kuelekeza macho zaidi barani Afrika, iliamuru Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akamatwe mwaka 2023. Alitajwa na Mahakama hiyo kufanya uhalifu wa kivita na kuwatumia watoto katika vita yake na Ukraine.

ICC haina vyombo vya dola na badala yake hutegemea nchi husika kumkamata mashitakiwa na kumfikisha makao makuu ya Mahakama hiyo mjini The Hague.

Kukosekana kwa Marekani kuneziachia mzigo nzito Uingereza, Japan, Ujerumani na Ufaransa, ambazo ndizo nchi zinazochangia fedha nyingi katika uendeshaji wa Mahakama hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img