CONAKRY, Guinea
RAIA wa Guinea wameshangazwa na gharama kubwa ya fomu ya kuwania urais iliyotangazwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Desemba, mwaka huu.
Gharama ya fomu ya kuwania kiti cha urais imetangazwa kuwa ni Dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh mil. 248 za Tanzania).
Guinea imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu Kanali Mamady Doumbouya alipoingia Ikulu kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021.
Taarifa za bei kubwa ya fomu ya urais zinakuja wakati nchi hiyo ikijiandaa kuunda kuachana na utawala wa kijeshi kwa kuunda Serikali ya kiraia.
Wachambuzi wa siasa wamesema hatua ya kupandishwa kwa bei ya fomu imelenga kuwazuia raia wengi kujitosa kuwania kiti cha urais.
“Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa,” amesema mchambuzi Kabinet Fofana katika mahojiano yake na BBC.
Hata hivyo, mamlaka zimejibu madai hayo zikisema kiasi cha fedha kimewekwa ili kuhakikisha ni wagombea wenye sifa pekee wanaoingia kwenye kinyang’anyiro.
Published:


