YOUNDE, Cameroon
MAHAKAMA Kuu nchini Cameroon imesisitiza kuwa haina mpango wa kufuta Uchaguzi Mkuu, na badala yake itatangaza matokeo ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo.
Kwa sasa, kumekuwapo na maandamano katika miji mikubwa ya Cameroon, ambapo wapinzani wanalalamikia kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu huo wa Oktoba 12, mwaka huu.
Hata hivyo, Mahakama ya Katiba ya Cameroon imejibu madai hayo ikisema bado hakuna ushahidi wa kuvurugwa kwa Uchaguzi.
Hivi karibuni, mgombea urais wa upinzani, Issa Tchiroma Bakary, alijitangaza kuwa ndiye mshindi mbele ya Paul Biya anayewania awamu ya saba madarakani akiwa na umri wa miaka 92.
Akijitangazia ushindi, Tchiroma Bakary alisema amempiku Biya kwa asilimia 55.
Biya amekuwa madarakani kwa miaka 43 na ilishangaza wengi kuona amefanya mkutano mmoja tu wa kampeni katika Uchaguzi wa mwaka huu.
Tchiroma Bakary (76), amewahi kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na sasa anamkabili bosi wake wa zamani katika kinyang’anyiro cha urais.
Published:


