12.5 C
New York

Kiongozi wa upinzani Odinga afariki

Published:

NAIROBI, Kenya
TAARIFA kutoka India alikokuwa akiendelea na matibabu zimeeleza kuwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameiaga dunia.
Odinga (80), amefariki kwa shambulio la moyo, kwa mujibu wa taarifa ya Hospitali aliyokuwa akitibiwa ya Devamatha kupitia Shirika la Habari la AP.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini India, Odinga aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya, alianguka ghafla alipokuwa akitembea na dada, binti na daktari wake.
Kwa mara ya kwanza, Odinga aligombea kiti cha urais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1997, ambapo alishika nafasi ya tatu nyuma ya Rais Daniel arap Moi na Mwai Kibaki.
Baadaye, alianzisha Chama chake cha National Development Party (NDP), hatua iliyokuja alipokwaruzana na wanasiasa wenzake wa FORD–Kenya.
Katika miaka ya hivi karibuni, mwanasiasa huyo atakumbukwa kwa majaribio yake matatu ya kugombea kiti cha urais katika chaguzi za 2013, 2017 na 2022.
Kwa mwaka In 2013, alishindana na Uhuru Kenyatta, ambapo alifikia hatua ya kupinga matokeo ya uchaguzi, ingawa alishindwa mahakamani.
Mwaka 2022, Odinga akiwa mwakilishi wa Muungano wa upinzani wa ‘Azimio la Umoja’, alipoteza nafasi nyingine ya kwenda Ikulu mbele ya William Ruto.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img