12.5 C
New York

Jeshi laingia Ikulu Madagascar, lavunja Tume ya Uchaguzi

Published:

ANTANANARIVO, Madagascar
JESHI nchini Madagascar limethibitisha kuingia Ikulu na kuchukua rasmi majukumu ya kuunda Serikali ili kuiongoza nchi hiyo.
Ikumbukwe, taarifa hiyo inakuja baada ya Rais Andry Rajoelina kukimbilia mafichoni akipaita kuwa ni sehemu salama kwa maisha yake.
Kupitia hotuba yake katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Rajoelina alisema amelazimika kuikimbia Ikulu baada ya kubaini kuwa viongozi wa jeshi walikuwa na mpango wa kumuua.
Chanzo cha matatizo yote hayo ni maandamano makubwa ya vijana wa Madagascar wanaoshinikiza Rajoelina kujiuzulu kutokana na kushindwa kumaliza kero za muda mrefu.
Sasa, akihutubia Taifa akiwa Ikulu jana, kiongozi wa jeshi, Michael Randrianirina, amesema wataunda serikali ya muda, kisha Uchaguzi utafanyika miaka miwili ijayo.
Pia, hatua hiyo ya kuchukua madaraka imeenda sambamba na kuvunja baadhi ya taasisi za kidemokrasia, ikiwamo Tume ya Uchaguzi wa nchi hiyo.
Katika hatua nyingine, mitaa mingi imeshuhudia maandamano makubwa ya vijana wakishangilia Rais Rajoelina kuondoka madarakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img