12.5 C
New York

Upinzani wajitangazia ushindi Uchaguzi Mkuu Cameroon

Published:

GAROUA, Cameroon
MGOMBEA wa urais kupitia upinzani, Issa Tchiroma, amejitangaza kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 12, mwaka huu.
Hata hivyo, wakati Tchiroma akichukua hatua ya kujiita mshindi, Tume ya Uchaguzi haijamtangaza mgombea alishinda kiti cha urais.
Aidha, Tchiroma mwenye umri wa miaka 76, ambaye aliwahi kuwa Msemaji wa Serikali na Waziri wa Ajira, amemtaka Rais Paul Biya kukubali matokeo.
Biya (92), ambaye ndiye rais mwenye umri mkubwa zaidi duniani akiwa ameiongoza Cameroon kwa miaka 43, anasaka muhula wake wake wa nane madarakani.
Kwa upande wake, Tchiroma amesema Biya anapaswa kukubali kushindwa kwa heshima ya boksi la kura na wananchi wa Cameroon.
“Ushindi wetu uko wazi na unapaswa kuheshimiwa,” amesema Tchiroma katika hotuba yake kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook. “Watu wamechagua na chaguo lao linapaswa kuheshimiwa.”
Aidha, Tchiroma aliwapongeza wapiga kura kwa kujitoa, hasa kwa uamuzi wao wa kukesha usiku wa jana wakilinda kura katika vituo.
“Pia, niwapongeze wagombea wenzangu, ambao wamenitumia jumbe za kunipongeza na kutambua nguvu ya watu.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img