12.5 C
New York

Rais Madagascar aikimbia Ikulu akihofia jeshi kumuua

Published:

ANTANANARIVO, Madagascar
RAIS wa Madagascar, Andry Rajoelina, ameibuka na kusema yuko sehemu salama zaidi na si Ikulu ili kunusuru maisha yake baada ya kushitukia mpango wa kuuawa.
Rajoelina amelazimika kuingia mafichoni, huku maandamano makubwa ya vijana yakiendelea kushinikiza ajiuzulu.
Akihutubia Taifa kupitia mtandao wa Facebook jana, Rajoelina mwenye umri wa miaka 51 amedai kuwa kwa sasa yuko mafichoni baada ya kugundua kuwa wasaidizi wake wanataka kumuua.
Kwa mujibu wa Rajoelina, mpango wa kumuua umesukwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa jeshi kwa kushirikiana na wanasiasa.
“Tangu Septemba 25, kumekuwapo na majaribio ya kuniua na kupindua Serikali. Kundi la wanajeshi na wanasiasa walipanga kuniua. Imenilazimu kutafuta sehemu salama ili kujinusuru,” amesema.
Licha ya kutofichua makazi yake mapya, taarifa zinadai kuwa kiongozi ameondoka Madagascar kwa msaada wa ndege ya kijeshi ya Ufaransa.
Rajoelina ni kama amekwama katika kutuliza maandamano yanayoendelea kwani hatua yake ya kuvunja baraza la mawaziri ilifeli baada ya vijana walimgeukia wakimtaka kung’oka madarakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img