25.9 C
New York

Mashambulizi ya Urusi yakata umeme Ukraine

Published:

KYIV, Ukraine
MAENEO mengi ya Mji Mkuu wa Kyiv yamekosa umeme kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na Urusi nchini Ukraine.
Mamlaka za Kyiv zimeeleza kuwa licha ya jitihada za kurejesha umeme kwa raia 540,000, bado maeneo mengi yanakosa huduma hiyo muhimu.
Kwa upande wake, Meya wa Kyiv, Vitaliy Klitschko, aliongeza kuwa mashambulizi ya Urusi yamesababisha watu 12 kujeruhiwa.
Aidha, katika maeneo ya Kusini mwa Mji wa Zaporizhzhia, imeripotiwa kuwa kijana mwenye umri wa miaka saba amepoteza maisha na wengine saba kuachwa na majeraha.
Urusi iliyoivamia Ukraine mwaka 2022, imeendelea kuelekeza mashambulizi yake katika maeneo nyeti ya uchumi wa majira zake hao, ikiwamo miundombinu ya usafiri na nishati.
Hivi karibuni, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alizitaka jumuhiya za kimataifa kuingilia kati ubabe unaofanywa na Urusi akiuita kuwa ni ugaidi dhidi ya watu wake.
“Kinachotakiwa kwa sasa si maneno, bali hatua kutoka kwa Marekani, Ulaya na G7 (Umoja wa nchi saba tajiri duniani) kwa kusaidia ulinzi wa anga na kuweka vikwazo (dhidi ya Urusi),” alisema Zelensky.

Related articles

Recent articles