RABAT, Morocco
POLISI nchini Morocco wanawashikilia vijana zaidi ya 60 katika maandamano yanayoendelea miji mikubwa, ikiwamo Rabat na Casablanca.
Maandamano hayo, ambayo asilimia kubwa ya washiriki wake ni vijana yanashinikiza mabadiliko makubwa katika sekta za elimu na afya.
Mamlaka za ulinzi na usalama zilijitihahidi kuzuia maandamano hayo tangu yalipoanza kuhamasishwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko mitandaoni.
Madai makubwa ya vijana nchini Morocco yanalenga kukosoa hatua ya Serikali kuwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa viwanja vya soka, huku ikipuuzia sekta muhimu za afya na elimu.
Itakumbukwa kuwa Morocco inajiandaa kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2030.
Mmoja ya waandamanaji amesikika akihoji: “Viwanja vya soka vipo, ziko wapi hospitali? Tunataka mfumo bora wa afya na uwajibikaji.”
Kiwango cha uhaba wa ajira nchini Morocco ni asilimia 12.8, huku asilimia 35.8 ikiwahusu wahitimu wa elimu ya juu, kwa mujibu wa Shirika la Takwimu la Taifa hilo.
Published:


