13.1 C
New York

Waandamana kupinga mauaji ya wasichana watatu

Published:

BUENOS AIRES, Argentina
MAELFU ya raia wa Argentina wameingia mitaani kulaani mauaji ya wasichana watatu.
Katika video iliyozua taharuki baada ya kupostiwa mitandaoni, wasichana hao wanaonekana wakiteswa na kisha kuuawa.
Wikiendi hii, maelfu ya raia wameandamana katika mitaa ya Mji Mkuu, Buenos Aires, wakiishinikiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya wahusika.
Baadhi ya waandamaji wameonekana wakiwa na mabango yenye majina ya wasichana nao, ambao ni Morena Verdi na Brenda Del Castillo (20) na Lara Gutierrez (15).
Kwa upande wake, baba mzazi wa Del Castillo, Leonel, alikuwa sehemu ya maandamano, ambapo amesema: “Wanawake wanapaswa kulindwa kuliko kipindi chote kile.”
Wakati huo huo, polisi wanawashikilia watu watano wakihusishwa na tukio hilo la mauaji.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img