13.9 C
New York

Vijana 20 waokolewa wakipelekwa vitani Ukraine

Published:

NAIROBI, Kenya
POLISI nchini Kenya wamewaokoa vijana wake zaidi ya 20 waliokuwa wakipelekwa Urusi kwa ajili ya kusafirishwa hadi Ukraine.
Taarifa ya polisi inasema vijana hao waliahidiwa ajira nzuri Urusi lakini lengo lilikuwa ni kupelekwa Ukraine na kutumiwa katika uwanja wa vita.
Baada ya polisi kufuatilia na kuunasa mtandao uliokuwa ukiwasafirisha, waliwakuta vijana hao wakiwa na nyaraka za kusafiria, sambamba na barua za kazi.
Mmoja ya washukiwa wa mtandao huo amefunguliwa na mashitaka, akielezwa kuwa ndiye anayeratibu safari hizo za Septemba na Oktoba, mwaka huu.
Baada ya kufikishwa mahakamani, mshukiwa huyo atashikiliwa kwa siku 10 ili polisi waendelee na uchunguzi dhidi yake.
Kwa siku za hivi karibuni, zimekuwapo taarifa nyingi juu ya usafirishaji haramu nchini Kenya.
Hivi karibuni, mwanamichezo chipukizi alikamatwa nchini Ukraine na kusema alifika huko baada ya kupelekwa Urusi akiahidiwa ajira nzuri jeshini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img