11.8 C
New York

Urusi yaua watatu, yajeruhi 24 Ukraine

Published:

KYIV, Ukraine
SHAMBULIZI la asubuhi ya leo lililofanywa na Urusi nchini Ukraine mjini Kyiv limesababisha vifo vya watu watatu, akiwamo mtoto.
Aliyethibitisha kutokea kwa shambulio hilo ni Meya, Vitali Klitschko, ambaye amesema watu 24 walijeruhiwa.
Mtoto aliyepoteza maisha ni binti wa miaka 14, pia ikielezwa kuwa watoto watano walijeruhiwa.
Wakati huo huo, katika shambulizi hilo, jengo la ghorofa tano liliangushwa, pia ikisababisha moto uliovamia makazi ya watu wilayani Dnipro.
Aidha, majanga hayo yanakuja zikiwa ni siku chache tu tangu shambulizi la anga la Urusi liliposababisa watu zaidi ya 100,000 kukosa makazi nchini Ukraine.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img