LOS ANGELES, Marekani
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump, ajenga ikiwa ni namna ya kumaliza mgogoro wa Gaza.
Blair amekuwa mjumbe muhimu katika kutafuta suluhisho la vita kati ya Israel na Palestina tangu alipoondoka katika nafasi ya Waziri Mkuu mwaka 2007.
Hatua ya kiongozi huyo kuingia Ikulu ya Marekani na kukaa mezani na Trump inakuja baada ya Israeli kutishia kuivamia kwa ‘nguvu zote’ Gaza.
Tayari wanajeshi wa Israel wameripotiwa kuanza hatua hiyo, ambapo maelfu ya raia wa Palestina wamelazimika kuyakimbia makazi yao.
Israel imefanya hivyo, licha ya jumuhiya za kimataifa, ukiwamo Umoja wa Mataifa (UN) kukosoa uamuzi wa kuivamia Gaza.
Wakati huo huo, hatua ya Israel kusitisha misaada iliyokuwa ikipeleka Gaza imeendelea kusababisha vifo, hasa kwa upande wa watoto na wazee.
Published:


