13.1 C
New York

Chart| Sababu kuu zinazowafanya watu kutumia Intaneti

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Takwimu kutoka Global Web Index (GWI) zinaonyesha kuwa miongoni mwa watumiaji wa intaneti duniani wenye umri wa miaka 16 na kuendelea, sababu kubwa zaidi inayowasukuma kutumia huduma hiyo ya mtandao ni kusaka taarifa ambapo asilimia 61.3 ya watu wanasema ndiyo sababu kuu inayowasukuma kutumia mtandao.

Sababu nyingine maarufu ni kuwasiliana na marafiki na familia (58.8%), kuangalia video, vipindi au filamu (55%), na kufuata habari na matukio (53.3%). Aidha, zaidi ya nusu ya watumiaji hukitumia kupata maelekezo ya jinsi ya kufanya mambo mbalimbali (50.1%).

Utafiti huo unaonyesha kuwa matumizi ya injini za utafutaji (search engines) ni ya juu sana katika makundi yote ya umri na jinsia, huku hata wastaafu wakiongoza kwa kutumia njia hiyo kutafuta taarifa.

Kwa jumla, kati ya watumiaji bilioni 5.65 wa intaneti duniani, karibu wote wanashiriki katika shughuli za kusaka maarifa, kuwasiliana, kujiburudisha na kufanya utafiti kuhusu bidhaa, afya, safari na masuala ya kifedha. Ukiangalia mtindo huu, ni wazi kuwa intaneti imekuwa nyenzo muhimu ya kila siku kwa karibu kila mtu, bila kujali umri au jinsia.

Endelea kukaa karibu na www.gazetini.co.tz kwa mengi zaidi

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img