Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Mwimbaji anayekuja kwa juu kwenye muziki wa Injili nchini, Betty Malange, amewashukuru mashabiki kwa mapokezi makubwa ya wimbo wake unaoitwa Maajabu alioutoa hivi karibuni.
Akizungumzia wimbo huo, Betty amesema amepokea mrejesho mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Injili ambao wamebarikiwa na ujumbe wa Maajabu huku wengi wakimuona Mungu kwa viwango vikubwa.
“Nashukuru wimbo wangu umegusa maisha ya watu, Mungu ameendelea kunitumia kwa viwango vikubwa na hii ni hatua yangu ya mwanzo ya kuendelea kumtumikia Mungu kupitia uimbaji,” amesema Betty.
Ameongeza kwa kuwaomba mashabiki waendelee kumfuatilia kwenye mitandao yake mbalimbali ya kijamii hasa YouTube, Facebook, Instagram na Tiktok kwani mambo mengine mazuri yanakuja.


