11.6 C
New York

Syria, Israel kusitisha mapigano

Published:

JERUSALEM, Israel
MATAIFA ya Syria na Israel yamefikia makubaliano ya kusitisha vita, kwa mujibu wa Balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack.
Kwa mujibu wa balozi huyo ambaye ni mjumbe maalumu wa Marekani nchini Israel, mpango huo umesimamiwa na Uturuki, Jordan na mataifa mengine jirani.
Hatua hiyo ya kuweka chini silaha inakuja zikiwa ni siku chache tu tangu mashambulizi ya anga ya Israel yalipoishukia Syria na kuharibu majengo ya Serikali.
Mbali ya kuua watu watatu, moja ya video ilionesha jengo la Wizara ya Ulinzi likiwa limeshambuliwa.
Kwa miezi ya hivi karibuni, Marekani imeonekana ikifanya jitihada kubwa katika kumaliza mzozo huo.
Katika jitihada hizo, Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani, Marco Rubio, alimpigia simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, kujadili namna ya kuimarisha uhusiano wa Syria na Israel.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img