13.9 C
New York

Van Gaal: Nimepona saratani, narudi mzigoni

Published:

AMSTERDAM, Uholanzi

KOCHA mkongwe, Louis van Gaal, amesema amepona ugonjwa wa saratani na sasa yuko fiti kurejea katika majukumu yake.

Miaka mitatu iliyopita, Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 73 alitangaza kusumbuliwa na saratani.
Alitangaza hilo wakati huo akiwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uholanzi.

“Miaka miwili iliyopita, nilifanyiwa upasuaji mara kadhaa. Zilikuwa za hatari lakini zote zimefanya kazi.
“Nimekuwa nikifuatilia ila baada ya miezi michache na naendelea vizuri. Nazidi kuimarika siku baada ya siku,” alisema.

Kwa nyakati tofauti, Van Gaal aliwahi kuzinoa Ajax, Barcelona, Bayern Munich na Manchester United.
Aidha, kocha huyo ameweka wazi kuwa hatazamii kurudi kwenye klabu na badala yake anavutiwa kuzinoa timu za taifa. Kwa sasa, mkufunzi huyo ni mshauri wa klabu yake ya zamani ya Ajax.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img