LONDON, England
MAURICIO Pochettino ni miongoni mwa makocha waliokuwa kwenye usahili wakati Brentford ilipokuwa ikisaka kocha hivi karibuni.
Pochettino aliyewahi kufanya kazi Ligi Kuu ya England (EPL) akiwa na Southampton, Tottenham na Chelsea, kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Marekani.
Hata hivyo, licha ya ‘CV’ kubwa ya Muargentina huyo, ikiwamo kuinoa PSG, mabosi wa Brentford walimtangaza Keith Andrews kuwa kocha wao mpya.
Kwa upande mwingine, huenda taarifa hii ya kufanya usahili Brentford ikatibua uhusiano kati yake na mabosi wa Shirikisho la Soka la Marekani (USSF).


