11.6 C
New York

Pogba amwaga machozi akisaini Monaco

Published:

MONACO, Ufaransa

KATIKA video iliyosambaa mitandaoni, kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba, anaonekana akimwaga machozi wakati akisaini mkataba wa kujiunga na Monaco ya Ligue 1.

Jana, Monaco ilimpa mkataba wa miaka miwili nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni mshindi wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Ikumbukwe, Pogba anarejea baada ya miaka miwili ya kuwa nje ya soka la ushindani tangu alipokumbwa na sekeseke la kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Awali, staa huyo wa zamani wa klabu za Manchester City na Juventus alifungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne lakini alikata rufaa na adhabu hiyo kupungua na kubaki miezi 18.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img