9.5 C
New York

Zaidi ya washindi 400 wazawadiwa kupitia kampeni ya ‘Tamba na Bonasi’

Published:

Na Iman Nathaniel, Gazetini

Zaidi ya washindi 400 wamejishindia zawadi mbalimbali kupitia kampeni inayoendeshwa HaloPesa inayoitwa Tamba na Bonasi’.

Kupitia kampeni hiyo wateja wa HaloPesa wanapata nafasi ya kujishindia bonasi za papo kwa papo kila wanapofanya miamala kama vile kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, au kufanya malipo ya bidhaa.

Miongoni mwa washindi hao ni Selemani Khalfan, ambaye alijinyakulia zawadi ya Sh 1,000,000.

Akizungumza wakati wa kupongeza washindi hao, Ofisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, alisema kuwa kampeni ya Tamba na Bonasi ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuwashukuru wateja wake kwa kuendelea kuwaamini na kutumia huduma zao kwa wingi.

“Kampeni hii ni njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuamini kwa miaka tisa sasa. Kupitia HaloPesa, tumerahisisha maisha ya wateja wetu kwa huduma nafuu, salama na rahisi kutumia. Wateja wetu wana nafasi ya kushinda hadi milioni 2 kila siku, kila wiki na kila mwezi kutoka kwa Mr. Bonasi na kila muamala ni nafasi ya ushindi,” alisema Lwiza.

Aidha, aliongeza kuwa wataendelea kuboresha huduma ili kuhakikisha wateja wanafanya miamala kwa urahisi zaidi na kwa gharama nafuu.

Ametoa wito kwa wateja kuwa makini na matapeli, ikisisitiza kuwa mawasiliano rasmi kutoka Halotel au HaloPesa ni kupitia namba 100 pekee.

Lwiza amefafanua kuwa kampeni ya Tamba na Bonasi ni sehemu ya maadhimisho ya miaka tisa ya HaloPesa tangu kuanzishwa kwake, ikiashiria mafanikio makubwa katika kutoa huduma bora za kifedha kidijitali nchini Tanzania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img