20.9 C
New York

United wamaliza ‘uteja’ Anfield

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
BAO la mpira wa kichwa katika dakika ya 84 lililofungwa na Harry Maguire limeifanya Manchester United kupata ushindi wake wa kwanza katika mechi tano zilizopita ndani ya Uwanja wa Anfield.
Man United imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao, Liverpool, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Iliwachukua Man United dakika mbili tu za mchezo kupata bao la kuongoza kupitia kwa Bryan Mbeumo, kabla ya Cody Gakpo kusawazisha zikiwa zimebaki dakika 12 mchezo huo kumalizika.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa ‘Mashetani Wekundu’ kupata ushindi wakiwa Anfield tangu mwaka 2016.
Kwa upande wao, Liverpool wamepoteza mechi zote nne walizoshuka dimbani hivi karibuni.
Ikumbukwe, mara ya mwisho kwa Liverpool kukosa ushindi katika mechi nne mfululizo ilikuwa mwaka 2014, wakati huo kocha akiwa ni Brendan Rodgers.

Related articles

Recent articles