24.8 C
New York

Bafana Bafana kufuzu au kukosa Kombe la Dunia 2026?

Published:

DURBAN, Afrika Kusini
MASHABIKI wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ walijikuta kwenye majonzi baada ya ‘chama’ lao kulazimishwa suluhu na Zimbabwe katika mchezo wa jana.
Ni mechi ambayo walikuwa nyumbani katika Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban wakifukuzia tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwakani.
Sasa, baada ya Nigeria kuifunga Lesotho mabao 2-1 na Benin kuichapa Rwanda bao 1-0, mambo ni magumu kwa Bafana Bafana.
Kwa namna msimamo ulivyo, Benin wako kileleni wakiwa na pointi 17, huku Bafana Bafana wakiwa nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili.
Hivyo, ili Waafrika Kusini waione timu yao ikifuzu, ni lazima ipate ushindi na kukusanya pointi tatu katika mechi ijayo dhidi ya Rwanda.
Hata baada ya ushindi, lazima mashabiki wa Bafana Bafana waombe Nigeria ipate pointi tatu za mchezo wao dhidi ya Benin.
Kazi haitakuwa imekwisha. Baada ya hapo, Bafana Bafana italazimika kuifunga Rwanda na ndipo itapokuwa imejihakikishia tiketi ya kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Related articles

Recent articles